BOIPLUS SPORTS BLOG

Akram Msangi, Dar
KIKOSI cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kimejipanga kushinda mchezo wake wa mwisho wa kufuzu AFCON dhidi ya Nigeria utakaopigwa kesho licha ya kuwa hawatasonga mbele.

Mkuu wa msafara wa kikosi hicho Mussa Kisoki ameiambia BOIPLUS kuwa hali ya hewa ni mvua lakini wamejiandaa kuwakabili 'Super Eagles' kwa hali yoyote.

Kisoki alisema wachezaji wamejipanga kushinda na wana morali ya hali ya juu licha ya mchezo huo kuwa wa kukamilisha ratiba kwakua timu zote zimeshindwa kufuzu.

"Tumejipanga kushinda mchezo wetu wa mwisho, wachezaji wako salama na hakuna majeruhi yoyote tayari kwa mtanange huo," alisema Kisoki.

Katika mchezo wa awali uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1 huku Nigeria wakisawazisha dakika za mwishoni.

Kocha wa Stars Charles Boniface Mkwasa alisema atawatumia mabeki wa kati Andrew Vicent na David Mwantika baada ya Kelvin Yondani kushindwa kusafiri kutokana na matatizo ya kifamilia.

Post a Comment

 
Top