BOIPLUS SPORTS BLOG

Akram Msangi & Ally Shatry
 Laudit Mavugo na Mohamed Hussein wakimpongeza Ibrahim Ajibu(katikati) baada ya kuipatia timu ya Simba bao la kwanza dhidi ya Mtibwa jana

Beki wa Mtibwa Issa Rashid 'Baba Ubaya' (21) akimchunga kwa umakini mkubwa Kiungo wa Simba Shiza Kichuya anayemiliki mpira, kulia ni Haruna Chanongo

"Tunashuka wote kukaba", nahodha wa Mtibwa Shaban Nditi(4), mlinzi Ponera na mshambuliaji Kelvin Friday wakiwa wamejipanga kuweka ulinzi langoni mwao wakati Simba wakijiandaa kupiga kona

" Ulinzi Shirikishi" ......wachezaji watatu wa Mtibwa wakiongozwa na Salim Mbonde kushoto wakipambana kumdhibiti Mavugo

Kipa wa Mtibwa Abdallah Makangana akiwa amelala chini baada ya kushindwa kuudaka mpira wa kichwa uliopigwa na Ajibu

Kichuya akiwatoka Baba Ubaya na Ibrahim Jeba, wachezaji hawa walikuwa na Kichuya kwenye kikosi cha Mtibwa cha msimu uliopita

Fredrick Blagnon akimpongeza Ajibu

Wachezaji wa Simba wakishangilia bao la pili lililopachikwan wavuni na Mavugo 
Kikosi cha Mtibwa Sugar kilichoanza dhidi ya Simba jana

Kikosi cha Simba kilichoanza dhidi ya Mtibwa jana


BOIPLUS inawatakia Waislamu wote Heri na Baraka ya Eid.......

Post a Comment

 
Top