BOIPLUS SPORTS BLOG

KAMPALA, Uganda
TIMU ya Taifa ya wanawake ya Tanzania 'Twiga Stars' imeibuka mabingwa wa michuano inayoshirikisha nchi wanachama wa CECAFA baada ya kuichapa Kenya mabao 2-1 kwenye mchezo wa Fainali.

Michuano hiyo ambayo ndiyo imefanyika kwa mara ya kwanza katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati imeshuhudia Twiga wakiweka rekodi kwa kuibuka mabingwa wa kwanza.

Twiga ilipata bao la kwanza kupitia mshambuliaji Mwanahamisi Omari dakika ya 39 baada ya kuichambua safu ya ulinzi ya Kenya kabla ya kufunga bao maridadi.

Dakika tano baadae Mwanahamisi tena aliwanyanyua Watanzania kwenye viti baada ya kufunga bao la pili kwa mpira wa adhabu upande wa kushoto wa uwanja kutokana na mchezaji mmoja wa Kenya kufanya madhambi.

Kipindi cha pili Kenya walikuja juu kwa kulisakama lango la Twiga ambapo dakika ya 48 Christina Nafula aliipatia bao la kufutia machozi kufuatia mabeki ya Twiga kuzembea kuondoa hatari.

BOIPLUS inawapongeza mashujaa hao ambao wamelitoa Taifa kimasomaso katika medani ya soka kimataifa baada y1qa1a timu ya taifa ya wanaume 'Taifa Stars' na klabu zilizoshiriki michuano ya kimataifa kushindwa kufanya hivyo.

Post a Comment

 
Top