BOIPLUS SPORTS BLOG

KAMPALA, Uganda
HATIMAYE Afrika Mashariki imepata mwakilishi katika fainali za Mataifa ya Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Gabon baada ya Uganda kufuzu kufuatia ushindi wa bao 1-0 walioupata dhidi ya Comoro jioni ya leo jijini Kampala.

Uganda imefuzu kutoka kundi D kwa pointi 13 sawa na Burkinafaso waliowafunga Botswana mabao 2-1. Botswana wenyewe wamemaliza wakiwa na alama sita huku Comoro wakiburuza mkia na pointi tatu tu.

Bao pekee katika mchezo wa leo liliwekwa nyavuni na mshambuliaji Farouk Miya katika dakika ya 36 baada ya mashambulizi kadhaa langoni mwa Comoro.

Tayari Tanzania na Kenya zimeshindwa kufuzu kwa fainali hizo hivyo kubakia kuwa watazamaji tu.

Post a Comment

 
Top