BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
RAIS wa Shirikisho la mchezo wa mpira wa magongo duniani (IHF) Leandro Negre akiambatana na Rais wa Afrika wa mchezo huo Seif Ahmed wapo nchini kwa ziara ya kuisaidia Tanzania kufanya vizuri kimataifa.

Rais huyo alisema ataisaidia kujenga uwanja wa kisasa wa mchezo huo nchini huku Ahmed akiahidi miundombinu bora ya dimba hilo ili kuirudisha Tanzania katika ramani ya mpira wa magongo duniani kama ilivyokuwa miaka ya 1980.

"Nitasaidia kujenga uwanja wa kisasa wa mchezo huu likipatikana eneo tu nitatimiza ahadi yangu," alisema Negre.

Kwa upande wake Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Nape Nnauye amemshukuru Rais huyo kwa kudhamira yake ya kutaka kusaidia mchezo huo huku akiahidi kwa niaba ya Serikali kutoa ushirikiano mpaka kukamilika kwa ujenzi huo.

"Nina waahidi kwa niaba ya Serikali kutoa ushirikiano mpaka kukamilika kwa ujenzi huo ili kurejesha umaarufu nchini kama ilivyokuwa zamani," alisema Nape.

Timu ya mchezo huo inatarajia kushiriki kwenye michuano itakayofanyika mkoani Arusha ambayo itashirikishi nchi nane za Afrika baadae baada ya mipango kukamilika.

Post a Comment

 
Top