BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
WABUNGE wanaoshabikia timu za Simba na Yanga watakutana kwenye mchezo maalum wa kuchangia Watanzania waliopatwa na madhara ya tetemeko la ardhi mkoani Kagera mtanange utakaopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Septemba 25.

Mapato yatakayo patikana katika mchezo huo pamoja na ile iliyochangwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania shilingi milioni 85 zitaenda moja kwa moja kwa wahanga wa tetemeko hilo ili iweze kuwasaidia.

Mwenyekiti wa Bunge Sports Club William Ngeleja amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kuchangia kupitia mchezo huo ili waliopatwa na majangwa waweze kupata misaada.

"Tatizo lililotokea ni kubwa na Serikali pekee haiwezi ni lazima Watanzania tujitokeze kwa wingi ili kuhakikisha tunaweza kuwasaidia wenzetu waliopatwa na majanga," alisema Ngeleja.

Wabunge wa Simba wataongozwa na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa ambaye anacheza winga ya kulia huku upande wa Yanga wakimtegemea Waziri wa Mambo ya ndani Mwigulu Nchemba kuongoza safu ya ushambuliaji.

Mchezo huo utatanguliwa na mechi kati ya wasanii wa Bongo Fleva na Bongo Movies huku timu ya Bunge Netball wakicheza na TBC Queens.

Viingilio katika mchezo huo ni:
Mzunguko shilingi 3000
VIP C  shilingi 10000
VIP B  shilingi  15000
VIP B  shilingi  50000
VIP A  shilingi  100,000
Kwenye viti ninavyo mzunguka Mgeni rasmi atakaye taka kukaa atalipia milioni moja.

Post a Comment

 
Top