BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
WABUNGE wanaoshabikia timu ya Yanga wamewabugiza wenzao wa Simba kwa mabao 5-2 kwenye mchezo wa hisani kuchangia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo ambao Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa alikuwa mgeni rasmi, Yanga walionekana kuwazidi Simba karibuni kila idara ambapo Ridhiwani Kikwete ya Yanga alikuwa mwiba mkali.

Sadifa Hamisi aliipatia Yanga bao la kwanza dakika ya tatu kabla ya Mohamed Mchengerisa hajafunga mabao mawili ya haraka dakika ya 5 na 8.

Cosato Chami aliifungia Simba bao la kwanza dakika ya 18 kabla ya Mwigulu Nchemba kuongeza mabao ya haraka kwa Yanga dakika ya 25 na 28.

Kaiza Makame aliipatia Simba bao la pili kwa mkwaju wa penati dakika ya 39 baada ya mchezaji mmoja wa Wekundu hao kufanyiwa madhambi katika eneo la hatari.

Matokeo mengine Wasanii wa Bongo fleva waliwafunga Bongo Bovies kwa changamoto ya mikwaju ya penati 5-4 baada ya kutoka sare ya kufungana bao 1-1 katika muda wa kawaida.


Bongo Movies ndio walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 11 kupitia kwa Nteze kabla ya H baba kusawazisha dakika ya 17.

Kwa upande wa Netball timu ya Wabunge Wanawake waliwafunga TBC vikapu 15 -14.

Mapato yaliyopatikana ni sh 187 milioni 187 ambapo pesa zote zitapelekwa kwa wahanga kama ilivyopangwa.

Post a Comment

 
Top