BOIPLUS SPORTS BLOG

MADRID, Hispania
MABINGWA watetezi wa klabu Bingwa barani Ulaya Real Madrid imeanza vyema harakati za kutetea taji hilo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1dhidi ya Sporting CP kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu.

Wageni ndiyo walikuwa wakwanza kupata bao dakika ya 48 kupitia kwa Bruno Cesar kabla ya wenyeji kusawazisha kupitia kwa Cristiano Ronaldo dakika ya 89.

Mshambuliaji aliyerejea kwa miamba hiyo akitokea Juventus Alvaro Morata aliwapatia wababe hao wa jiji la Madrid goli la ushindi dakika ya 90 na kuwahakikishia kuondoka na alama zote tatu.

Matokeo mengine ya mechi za Klabu Bingwa zilizochezwa jana.


Manchester City 4 - 0 Borussia M'gladbach.

Bayer Leverkusen 2 - 2 CSKA Moskva

Tottenham Hotspur 1 - 2 Monaco

Legia Warszawa 0 - 6 Borussia Dortmund

Club Brugge 0 - 3 Leicester City

Porto 1 - 1 København

Olympique Lyonnais 3 - 0 Dinamo Zagreb

Juventus 0 - 0 Sevilla

Post a Comment

 
Top