BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi Wetu, Shinyanga
MABINGWA wa kusakata kabumbu Tanzania, Yanga ya jijini Dar es Salaam leo imekubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Stand United mchezo wa ligi kuu ya Vodacom uliochezwa kwenye dimba CCM Kambarage mjini Shinyanga.

Kipindi cha kwanza ambacho kilikuwa cha kasi kilimalizika huku ikishuhudiwa timu zote mbili zikitoka bila bao lolote licha ya kosa kosa nyingi zilizotokea.

Yanga walionekana kumiliki mpira kwa kiasi kikubwa huku wakitumia zaidi pasi ndefu baada ya viungo wa Stand kumudu kuharibu mipango yote iliyokuwa ikifanyika katika eneo katikati ya uwanja.

Dakika ya 60 straika wa Stand alikatiza katikati ya walinzi wa Yanga Vicent Bossou na Haji Mwinyi kabla hajaachia shuti la chini chini ambalo lilimshinda mlinda mlango wa Yanga Ally Mustapha 'Barthez" na kuwa bao pekee katika mchezo huo.

Kwa matokeo hayo Yanga imebakiwa na pointi zake 10 ikiwa iko nyuma kwa mchezo mmoja wa kiporo ili ifanane na Simba inayoongoza ligi hiyo kwa pointi 16.

Post a Comment

 
Top