BOIPLUS SPORTS BLOG

Karim Boimanda
STRAIKA wa zamani  wa Azam FC mkenya Allan Wanga leo ameiwezesha timu yake mpya ya Tusker FC kutwaa ubingwa wa GOTV baada ya kuifungia bao pekee dhidi ya Ulinzi katika mchezo wa fainali uliopigwa kwenye dimba la Nyayo.

Wanga ambaye hakuwa akipata nafasi sana kwenye kikosi cha Azam kabla hawajakubaliana kuvunja mkataba, alifunga bao hilo dakika 32 akimalizia pasi ya Mandela aliyepenyezewa mpira kiufundi na Osborne Monday.

Kipindi cha kwanza kilimalizika Tusker wakitoka kifua mbele kwa bao hilo moja huku kipindi cha pili kikiwa cha kosakosa nyingi ambazo hazikuzaa bao lolote.

Ushindi huo umewapa ubingwa wa 23 watengeneza bia hao huku Ulinzi wakilazimika kusubiri hadi msimu ujao kutimiza ndoto yao ya kubeba kombe.

Post a Comment

 
Top