BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
HALI si shwari ndani ya  timu ya Azam FC baada kushindwa kupata matokeo mazuri katika mechi zao za mwanzo za muendelezo wa ligi ya Vodacom baada ya kukukusanya pointi 11 wakiwa nafasi ya nane huku Simba ndiyo ikiwa kinara wa ligi ikikusanya pointi 20.

Katika michezo nane iliyoshuka dimbani Azam imeshinda mechi tatu na kutoka sare miwili huku ikipoteza mitatu ambayo ni dhidi ya Simba (1-0), Ndanda FC (2-1) pamoja na Stand United jana (0-1).

Azam wamebadilisha benchi zima la ufundi ambapo sasa lipo chini ya Kocha Mhispania, Zeben Hernandez ambaye amekuja na watu wake kwa ajili ya kukinoa kikosi hicho kilichotwaa ubingwa msimu wa 2013/14 chini ya kocha Joseph Omog anayefundisha timu ya Simba msimu huu.

Hernandez ana kazi kubwa ya kufanya ndani ya kikosi hicho kwakua hali ya kujituma huku ikionekana morali ya wachezaji imeshuka pia wamekuwa wakiruhusu magoli mepesi kulinganisha na ilivyokuwa hapo awali.

Katika mchezo wa awali dhidi ya African Lyon uliomalizika kwa sare ya bao 1-1 Azam walirudisha bao dakika za majeruhi ambapo kama Lyon wangeongeza umakini katika safu ya ushambuliaji basi wangeweza kuibuka na ushindi wa zaidi ya mabao matatu.

Azam wamekuwa na idadi kubwa ya wachezaji majeruhi hasa katika safu ya ulinzi ambapo mabeki Agrey Morris, Erasto Nyoni pamoja na Pascal Wawa ambapo kuna baadhi ya mechi kiungo Himid Mao amekuwa akitumika kama beki wa kati.

Hata safu ya ushambuliaji inayoongozwa na nahodha John Bocco nayo haina makali na imekuwa akikosa magoli mengi msimu huu hali ambayo inamuweka kwenye mazingira magumu Kocha Hernandez na benchi lake la ufundi ambapo kuna dalili zinazoonesha uvumilivu utawashinda mabosi wa Azam.

Post a Comment

 
Top