BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi wetu
BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini Thomas Mashali 'Simba asiyefugika' ameuawa usiku wa kuamkia leo na watu wasiojulikana na mwili wake umeokotwa maeneo ya Kimara kabla ya kupelekwa Hospitali ya Taifa  Muhimbili.

Rais wa Oganizesheni ya Ngumi za kulipwa (TPBO) Yassini Abdallah 'Ustadh' alisema mauti yalimkuta bondia huyo baada ya kupigwa na watu wasiojulikana na mwili wake kuokotwa na wasamalia wema maeneo ya Kimara.

"Ni kweli Mashali amefariki dunia nimepokea Habari hiyo muda mfupi uliopita sasa nipo njiani naelekea Muhimbili" alisema Ustadhi.

Taarifa za utaratibu wa mazishi zitatolewa baadae na ndugu wa marehemu.

Post a Comment

 
Top