BOIPLUS SPORTS BLOG

MANCHESTER, Uingereza
TIMU ya Manchester United imekubali kichapo cha mbwa mwizi cha mabao 4-0 toka kwa Chelsea mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Old Trafford.

Katika mchezo huo Kocha Jose Mourinho alikutana na timu yake ya zamani ambayo alitimuliwa mwaka jana baada ya kushindwa kufanya vizuri ambapo mmiliki wake Roman Abromovich aliamua kumfuta kazi.


Chelsea ambayo inanolewa na Kocha Antonio Conte ilicheza kwa kasi zaidi na kutumia mashambulizi ya kushtukiza na kuwaacha United wakitawala mchezo lakini mwisho wa siku 'Mashetani Wekundu' hao walikubali kichapo hicho kikali cha mbwa mwizi.

Pedro ndiye aliyefungua karamu ya mabao dakika ya kwanza tu ya mchezo kabla ya Garry Cahill kuongeza la pili na kwenda mapumziko Chelsea wakiwa mbele kwa mabao 2-0.


Eden Hazard na Ngolo Kante waliongeza mengine mawili na kuwafanya United kuondoka vichwa chini wakishindwa kuamini kilichowakuta kwenye Uwanja huo maarufu kama Darajani.

United chini ya Mourinho wameshapoteza michezo mitatu ya ligi ambayo ni dhidi ya majirani zao Man City, Watford na Chelsea huku wakiwa na mtihani mwingine siku ya Jumatano kwenye dimba la Old Trafford dhidi ya City kwenye kombe la Capital One.

Post a Comment

 
Top