BOIPLUS SPORTS BLOG

TIRANA, Albania
MABINGWA wa kombe la dunia mwaka 2010 timu ya Taifa ya Hispania imeendeleza harakati zake za kutaka kuchukua ubingwa huo ambao Fainali zake zitafanyika nchini Urusi mwaka 2018 baada ya kuwafunga wenyeji Albania mabao 2-0.

Diego Costa aliwapatia wageni bao la kwanza dakika ya 55 baada ya kupokea pasi toka kwa David Silva kabla ya Nolito aliyetokea benchi kufunga la pili dakika ya 63.

Albania walizidiwa ujanja na mabingwa hao ambao walikuwa na nyota wao wengi wakiwemo Thiago Alcantara, Andres Iniesta, Costa, Silva pamoja na mlinda mlango David de Gea ambaye alikuwa likizo kwa muda mrefu wa mchezo kufuatia timu hiyo kumiliki mpira kwa muda mrefu.

Mchezo mwingine ulikuwa kati ya Macedonia dhidi ya Italia ambapo wenyeji walilala kwa mabao 3-2 huku Italia ambao ni mabingwa wa dunia mwaka 2006 wakitoka kwa shangwe.

Andrea Belotti ndiye aliyefungua pazia la mabao baada ya kuunganisha mpira wa kona uliopigwa na Marco Veratti dakika ya 24 kabla ya Cirlo Immobile kuongeza mengine mawili dakika ya 74 na 90.

Wenyeji walipata magoli yao kupitia kwa Ilija Netrovovski dakika ya 57 kabla ya Ferhan Hassan kuongeza la pili dakika mbili baadae.

Matokeo mengine:
Wales 1-1 Georgia
Moldova 1-3 Ireland
Serbia 3-2 Australia
Israel 2-1 Leichtenstein
Finland 0-1 Crotia
Ukraine 3-0 Kossovo
Iceland 2-0 Uturuki

Post a Comment

 
Top