BOIPLUS SPORTS BLOG

GENK, Ubelgiji
TIMU ya KRC Genk anayochezea mshambuliaji Mtanzania Mbwana Samatta imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Athletic Bilbao ya Hispania katika mchezo wa ligi ya  Europa uliofanyika kwenye uwanja wa Luminus Arena.

Beki wa kulia  Jacob Brabec aliwapatia goli la uongozi wenyeji hao baada ya kumalizia mpira uliopanguliwa na mlinda mlango wa Bilbao Herrerin kufuatia shuti kali la Nikos Karelis.

Onyinye Ndidi aliipatia Genk bao la pili dakika ya 83 kwa shuti kali nje kidogo ya eneo la hatari lililomshinda mlinda mlango wa Bilbao Herrerin.

Samatta ambaye aliianzia benchi aliingia dakika ya 56 kuchukua nafasi ya Thomas Buffel lakini alishindwa kuipatia bao timu yake kutokana na kubanwa vilivyo na mabeki wa Bilbao.

Matokeo mengine ya mechi za Jana

Man United 4-1 Fenerbahce
Fayernood 1-0 Zorya
Olympiacos 4-1 FC Astana
Young Boys 3-1 APOEL Nicosia
Mainz 05 1-1 Anderlecht
Saint Etiene 1-0 FK Qabala
AZ Alkmaar 1-2 Macab Tel Aviv
AS Roma 3-3 Austria Wien
Rapid Wien 1-1 Sasuolo

Post a Comment

 
Top