BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi wetu
MAAFISA wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA juzi walifanya ziara ya kushtukiza katika Ofisini za Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) zilizopo Ilala jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutaka kuzifunga kushinikiza kulipwa pesa za kodi zilizolimbikizwa.


TRA ilizifungia akaunti zote za TFF na kuchukuwa pesa zilizokuwepo lakini hazikutosha ambapo Shirikisho hilo lilitakiwa kulipa kwa wakati  mpaka ikafikia Mamlaka hiyo ikakamata magari matano na juzi walikuwa na dhamira ya kufunga ofisi lakini hawakufanya hivyo kwani walilipwa kiasi cha pesa kwa njia ya hundi.

TFF inadaiwa na TRA deni la sh 1.18 bilioni za kodi zilizolimbikizwa kwa muda mrefu ambapo mpaka sasa bado haijafahamika wameshalipa kiasi gani kwani walitakiwa kulipa kwa awamu kwa ajili ya kuhakikisha Wanamaliza na kuwa huru.

Ofisa Habari wa TFF Alfred Lucas ameiambia BOIPLUS kuwa Maofisa hao walifika hapo kwavile hakukuwa na mawasiliano mazuri ofisini kwao kwa sababu kuna malipo ambayo tayari yalikuwa yamefanyika ndiyo maana walifika lakini kwa sasa kila kitu kinaenda sawa.

 "Ni kweli jana (juzi) walikuja Maofisa wa TRA ila nadhani hakukuwepo na mawasiliano katika ofisi yao kwani tayari tumelipa hivyo hawakufanya jambo lolote," alisema Alfred.

Post a Comment

 
Top