BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi Wetu
SHIRIKISHO la Soka nchini (TFF) limefanya mabadiliko madogo ya ratiba kwa mechi za mwisho wa mzunguko huo ambazo zote zitachezwa mwezi ujao ikiwa ni wiki moja kabla ya kuanza kwa michuano ya Kombe la FA.

Novemba 9, kutakuwa na mechi kati ya Azam na Mwadui wakati Yanga na Ruvu Shooting mechi yao itachezwa Novemba 11 badala ya Novemba 10 huku Simba ikifunga mzunguko wa kwanza wa ligi Novemba 12 dhidi ya Prisons mechi itakayopigwa Uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya, ambapo awali walipangwa kucheza Novemba 9.

Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas alisema, "Ukomo wa mzunguko wa kwanza wa ligi ulitakiwa ufikie Novemba 6 lakini kutokana na mabadiliko yaliyokuwa yakitokea hapo kati basi ratiba imebadilika na sasa Simba ndiyo watafunga mzunguko huu, baada ya hapo kutakuwa na wiki ya FIFA na maandalizi ya mashindano mengine ikiwemo Kombe la FA,".

Yanga inaonekana ndiyo itakuwa na kibarua kigumu jijini Mbeya kwani Novemba 2, watacheza na Mbeya City na kumaliza dhidi ya Prisons mechi itakayochezwa Novemba 6 na baadaye kumaliza na Ruvu Shooting jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

 
Top