BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi wetu
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limepokea barua kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Ethiopia (EFF), ikielezea juu ya kufutwa kwa mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliokuwa ufanyike Oktoba 8, nchini humo.

EFF imesema kwamba imelazimika kufuta mchezo huo uliokuwa kwenye kalenda ya FIFA kwa sababu hali ya hewa si rafiki kwa sasa nchini Ethiopia kitu ambacho kingepoteza ladha ya mtanange huo.

Kwa barua hiyo, Kocha Mkuu wa Stars Charles Boniface Mkwasa atalazimika kuvunja kambi ya timu hiyo ambayo iliwekwa kwenye Hoteli ya Blue Peal iliyoko Ubungo, Dar es Salaam kuwavutia kasi Wahabeshi hao.

Mchezo huo uliratibiwa kwa mujibu wa kalenda ya shirikisho la soka Ulimwenguni FIFA ambalo huwa na kalenda ya wiki ya mechi za kimataifa kwa wanachama wake wakiwemo Tanzania na Ethiopia.

Ingekuwa ni faida kwa Stars  kama ingeshinda mchezo huo kwa maana kuna alama za nyongeza kama inatokea unaifunga timu mwenyeji lakini kufutwa mchezo inamaanisha hakutakuwa na mabadiliko makubwa kwa upande Tanzania katika viwango vya ubora vinavyotolewa na FIFA kila mwezi.

Matokeo yake yangekuwa ni sehemu malumu kupima viwango vya ubora na uwezo wa timu za taifa. Kwa sasa Tanzania inashika nafasi ya 132 kati ya nchi 205 wanachama wa FIFA zilizopimwa ubora. Ethiopia yenyewe inashika nafasi ya 126.

Post a Comment

 
Top