BOIPLUS SPORTS BLOG

Sheila Ally, Dar
MSIMU uliopita ulimalizika kwa kushuhudia hat-trick toka kwa wachezaji watatu ambao ni Ibrahim Ajib (Simba), Waziri Junior (Toto Africans) na Amissi Tambwe wa Yanga aliyepiga hat-trick mara mbili yaani katika mechi mbili tofauti na sasa Kelvin Sabato wa Stand United amefungua mlango wa mabao hayo.

Sabato alipiga hat-trick katika mchezo dhidi ya Mtibwa ikiwa ni ya kwanza kwenye ligi kuu ya Vodacom tangu msimu huu uanze huku timu nyingi zikiwa zimecheza mechi zaidi ya 10 ambapo Stand tayari imecheza mechi 12 na kukusanya pointi 21 zilizowaweka nafasi ya tatu ikishushwa na Yanga wenye pointi kama hizo ila ina mabao mengi ya kufunga.

Stand ilicheza na Mtibwa katika uwanja wa Manungu wilayani Turiani na kuambulia pointi moja baada ya kulazimisha sare ya bao tatu huku Sabato akifunga mabao yote ya Stand, Sabato aliondoka na mpira kama zilivyo kanuni kwa mchezaji atakayefunga hat-trick.

Akizungumza na BOIPLUS, Sabato alisema kuwa kupata ushindi ugenini ni kugumu ila walipambana kutokana na ushirikiano wao kitimu na ndiyo maana hata yeye aliweza kufunga mabao yote.

"Hii ni mara yangu ya kwanza kufunga mabao mengi kwenye mechi moja, nashukuru nimeweza hilo ila limewezekana kutokana na ushirikiano wetu kitimu peke yangu nisingeweza, mechi ilikuwa ngumu sana, Mtibwa walitaka kubaki na pointi tatu nyumbani hata sisi tulihitaji ushindi," alisema Sabato.

Post a Comment

 
Top