BOIPLUS SPORTS BLOG

MANCHESTER, Uingereza
KIUNGO Juan Mata ameibuka shujaa baada ya kuisaidia timu yake ya Manchester u
United kutoka kifua mbele katika ushindi wa bao 1-0 dhidi ya majirani zao Manchester City kwenye mchezo wa kombe la ligi mtanange uliopigwa Old Trafford.

United inayonolewa na Kocha Jose Mourinho waliingia uwanjani wakiwa na ari ya kusaka ushindi baada ya kuliweka lango City mashakani kwa muda mwingi wa mchezo lakini safu ya ushambuliaji ya Mashetani hao haikuwa na umakini wa kutosha.

Mata alifunga bao hilo pekee dakika ya 54 akimalizia kazi nzuri ya Zlatan Ibrahimovic upande wa kushoto ambaye aliwahadaa mabeki wa City kabla ya kupiga krosi safi ya chini chini iliyomkuta Mhispania huyo aliyeunganisha wavuni moja kwa moja.

Huu ni mchezo wa pili kwa Kocha Pep Guardiola kukutana na Mourinho tangu aanze kufundisha soka nchini Uingereza ambapo katika mchezo wa kwanza City iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 katika uwanja huo.

Mshambuliaji Sergio Aguero aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Nolito ambaye alishindwa kufurukuta kwenye ukuta wa United uliokuwa chini ya ulinzi wa Daley Blind na Marcos Rojo.

Matokeo mengine ya mechi za kombe la ligi

West ham 2-1 Chelsea
Southampton 1-0 Sunderland

Mechi zingine barani Ulaya;

Post a Comment

 
Top