BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi Wetu, Mbeya
KOCHA mkuu wa Mwadui FC amesema atajiuzulu kufundisha soka muda wowote kuanzia sasa kwavile amechoshwa na maamuzi mabovu ya marefarii wa hapa nchini.

Akizungumza kwa hasira baada ya kumalizika kwa mchezo ambao timu yake ilipigwa bao 1-0 na Mbeya City kwenye dimba la Sokoine jijini Mbeya, Julio alisema haoni sababu ya kuendelea kufundisha wakati tayari waamuzi wana matokeo yao.

"Natumia nguvu nyingi kufundisha, kampuni inatumia pesa nyingi kugharamia timu, tunasafiri safari ndefu halafu mwisho wa siku waamuzi wanafanya upendeleo wa waxiwazi.

"Nimeshachoka, nawatazama tu sasa na uamuzi wangu ni kuacha kufundisha mpira, na hii yaweza kuwa mechi yangu ya mwisho kuwa kocha," alisema Julio.

Bao pekee katika mchezo huo liliwekwa nyavuni na Ditram Nchimbi 'Ditinho' aliyeachia shuti kali lililomshinda kipa Shaban Kado na kutinga wavuni.

Mbeya City walitawala mchezo kwa kiasi kikubwa na kuwapoteza Mwadui ambao hawakuonyesha kandanda safi kama ilivyotarajiwa na wengi.

Post a Comment

 
Top