BOIPLUS SPORTS BLOG

Sheila Ally, Dar
KIPA wa Yanga, Beno Kakolanya hajawahi kusimama golini zaidi ya kukalishwa benchi au kutupwa jukwaani tangu asajiliwe na Hans Pluijm hadi ameondoka na sasa anakuja Mzambia, George Lwandamina ambapo ameanza kujipa matumaini mapya kuwa huenda kocha huyo atakuwa akimtumia.

Beno aliyetokea Prisons alikokuwa kipa namba moja,alisema kuwa hana haraka kupangwa kikosi cha kwanza ila anaamini ipo siku atapata nafasi hiyo kikubwa kwake ni kutoshusha kiwango chake huku akitazama zaidi mbinu za watangulizi wake Deo Munishi 'Dida' na Ally Mustafa 'Barthez'.

"Nimejifunza mambo mengi ndani ya Yanga, nimekuwa mvumilivu na nidhamu ikiwemo kujituma zaidi, naamini kocha ananiamini  mpaka sasa kwani mazoezini nafanya vizuri na anaridhika juu ya kazi yangu. Kutokudaka kwangu hakumaanishi kwamba kutanishusha kiwango, najiamini kwa kiasi kikubwa kutunza kiwango changu.

"Nilifika Yanga niliwakuta wenzangu (Dida na Barthez) wote wapo vizuri na ninachokifanya sasa ni kuwasoma zaidi mbinu zao ili nijifunze mengi kutoka kwao, nikipewa nafasi niitumie ipasavyo pasipo kuharibu, kujiamini ndo kila kitu na nina imani nitafanya vizuri  kazi yangu, nadhani kocha atakayekuja ataangalia mwenyewe nani anafaa kwake," alisema Beno.

Beno amekutana na upinzani mkubwa wa namba kwenye kikosi hicho ambapo amekuwa akikaa benchi endapo kipa mmoja wapo kati ya hao akiwa mgonjwa ama kuwa na matatizo yoyote binafsi.

Post a Comment

 
Top