BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
KESI iliyofunguliwa na mwanachama wa Yanga Frank Chacha dhidi ya klabu hiyo kuhusu kuzuia mkutano mkuu wa dharura uliokuwa ufanyike jana Oktoba 23 itatajwa kwa mara ya kwanza kesho katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Mwenyekiti wa klabu ya Yanga alipokea zuio la Mahakama lililowataka kutofanya Mkutano huo siku ya Ijumaa saa 1 jioni muda mfupi baada ya kuongea na Vyombo vya Habari akihamasisha Wanachama wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi ili kujadili masuala mbali mbali kuhusu maendeleo ya klabu hiyo.

Wiki iliyopita Chacha aliongea na Waandishi wa Habari kwenye mkutano ulioitishwa na Baraza la Wazee wa Klabu hiyo wakiongozwa na Mzee Ibrahim Akilimali alisema kuwa Mkutano huo ni batili kwakua umekiuka katiba ya Yanga na maamuzi yoyote ambayo yangefikiwa nayo yangekuwa batili kitu ambacho alikiri hakitaweza kutokea.


Chacha alisema kuwa hata Mkutano ule wa dharura wa kwanza uliofanyika Juni 6 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee ulikuwa batili kwakua uliitishwa bila Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo kutoshirikishwa chochote huku Wanachama wakiwa hawajapewa Ajenda hadi siku ya Mkutano kitu ambacho ni kinyume na Katiba ya Yanga.

Miongoni mwa Ajenda ambazo zingejadiliwa jana endapo kusingekuwa na zuio la Mahakama ilikuwa ni suala la ukodishwaji wa nembo ya Klabu kwa Kampuni ya Yanga Yetu inayomilikiwa na Manji hali iliyoleta mgawanyiko baina ya Wanachama ambao wapo wanaokubali na wengine wanapinga.

Post a Comment

 
Top