BOIPLUS SPORTS BLOG

Zainabu Rajabu,Dar
MASHABIKI wa Simba na Yanga wameilamikikia Serikali kuhusu mfumo wa upatikani wa tiketi za kielektroniki  za kuingilia Uwanjani kuwa haukupaswa kuanza kutumika kwenye mchezo wa leo wa Watani wa jadi.

Wakizungumza na BOIPLUS Mashabiki hao ambao wamefika uwanjani hapo tangu saa moja asubuhi walisema walisumbuka sana katika kupata tiketi hizo hali iliyopelekea misururu mikubwa ya watu.

Mfumo wa tiketi za Kielektroniki umeanza kutumika rasmi leo katika mchezo huu ambao una mashabiki wengi kutoka Dar es Salaam na mikoa ya jirani.

"Tumesumbuka sana toka juzi upatikanaji wa tiketi ni mgumu  mashine za kutolea ziko taratibu sana hali inayopelekea misururu mrefu," walisikika mashabiki hao.

Mashabiki hao wamefika mbali zaidi  na kusema kuwa wanaiomba serikali kurudisha mfumo wa zamani ili kuepusha usumbufu unaojitokeza katika ukataji wa tiketi hizo za kieletroniki.

Hata hivyo ombi hilo haliwezi kufanyiwa kazi kwavile tayari Serikali imeshasema kuwa ipo tayari kupambana na changamoto zote huku ikiwasihi watakaojaribu kuuhujumu mfumo huo.

Post a Comment

 
Top