BOIPLUS SPORTS BLOG

Sheila Ally, Dar
KOCHA wa Stand United, Patrick Liewig ameondoka nchini kurudi kwao Ufaransa ingawa ameacha maswali mengi kwa wadau wa soka wakidai kuwa ameondoka kwenye klabu hiyo na kwenda kusikojulikana lakini ukweli ni kwamba amerudi kwao kutatua matatizo ya kifamilia.

Mbali na matatizo hayo lakini pia imeeelezwa kwamba Visa ya Mfaransa huyo imebaki wiki moja kumalizika hivyo anapaswa kushughulikia ili aweze kuendelea kuishi nchini wakati anamalizia makubaliano ya mkataba wake ambao unakoma mzunguko huu wa kwanza wa ligi kuu.

Awali kocha huyo waliingia makubaliana na uongozi wa klabu hiyo kuvunja mkataba wake ambao alitakiwa kuusaini Septemba 26 lakini hakusaini baada ya kukubali kubaki hadi mzunguko huu umalizike na aliondoka nchini baada ya Stand kucheza na Mbeya City jijini Mbeya.

Mratibu wa timu hiyo, Mbasha Matutu aliiambia BOIPLUS kuwa "Kocha ameaga wala hajatoroka kama watu wanavyodai, yupo kwao na amesema atarudi ingawa hatujui ni lini, bado hatujamalizina naye hivyo ni lazima arudi kufuata haki zake kama hataki kuendelea na timu na si vinginevyo, asiporudi basi yeye atakuwa ameamua kuondoka mapema.

"Walivyotoka Mbeya ndiyo na yeye alipaswa kuja huku Shinyanga lakini alipiga simu kutueleza matatizo yake ya kifamilia na ukinzingatia pia Visa yake inamalizika Oktoba 23, wenzetu huwa hawapendi usumbufu hivyo huenda atashughulikia na hili kwani sisi tulimtafutia kibali cha kufanya kazi na makazi tu," alisema Mbasha

Leiwig ambaye timu yake sasa inafanya vizuri na inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 20 alikubali kuvunja mkataba wake kwankulipwa fidia ya dola 10,000 baada ya uongozi huo kueleza kushindwa kulipa gharama zake kutokana na wadhamini wao Acacia kujiondoa.

Post a Comment

 
Top