BOIPLUS SPORTS BLOG

LIVERPOOL, Uingereza
MANCHESTER United imeibana mbavu Liverpool baada ya kuilazimisha sare ya bila kufungana kwenye mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza uliopigwa kwenye uwanja wa Anfield hiyo ikiwa ni siku moja baada ya Azam na Yanga za hapa nchini kutoka sare tasa pia kwenye mechi ya ligi kuu ya Vodacom.

Vijana hao wa Kocha Jose Mourinho waliingia uwanjani wakiwa na lengo la kufanya mashambulizi ya kushtukiza huku wakiwa makini na vijana wa Jurgen Kloop kutokana na kasi waliyokuwa nayo nyota hao wenye vimo vifupi.

United walikuwa bora zaidi dakika 45 za kipindi cha kwanza kuanzia kwenye ulinzi na walicheza kwa nidhamu kwa ajili ya kuwadhibiti Daniel Sturridge, Roberto Firmino pamoja na Andrew Coutinho ambaye hakuwa kwenye kiwango chake baada ya kupoteza pasi nyingi.Kipindi cha pili Liverpool walirudi kwa kasi na kufanya mashambulizi kadhaa langoni mwa United lakini safu ya ulinzi ya Mashetani hao ilikuwa makini kuhakikisha nyavu zao hazitikiswi.

Dakika ya 72 kipa wa United David De Gea aliokoa shuti kali la mita 25 lililopigwa kwa ufundi na Coutinho ambalo lilikuwa likielekea wavuni lakini Mhispania huyo alikuwa makini langoni.

Liverpool wamefikisha alama 17 wakiwa nafasi ya nne baada ya kucheza mechi 8 huku United wakifikisha pointi 14.

Post a Comment

 
Top