BOIPLUS SPORTS BLOG

Zainabu Rajabu,Dar
BAADA ya kuifungia timu yake ya Yanga mabao 50 winga Saimon Msuva sasa anafikiria kwenda kucheza soka la kulipwa nje ambapo tayari ameanza kufanya michakato na moja ya timu ambayo hakutaka kuiweka wazi.

Msuva ambaye alifungia Yanga bao lake la kwanza mwaka 2013 dhidi ya URA ya Uganda ametoa wito kwa wadau kutomfananisha na washambuaji wa Yanga, Amissi Tambwe pamoja na Donald Ngoma.


Akizungumza na BOIPLUS alisema kuwa, "Nipo katika mazungumzo na timu moja ya nje  ila ni mapema mno kuitaja, muda ukifika kila kitu nitakiweka wazi." Msuva pia alifafanua kuhusu kutajwa kwake kutua Simba ambako ni muendelezo wa shutuma anazotupiwa na baadhi ya wadau wa Yanga kuwa ana mapenzi na wekundu hao, huku mara kadhaa akituhumiwa kucheza chini kila timu hizo zinapokutana.


"Kucheza chini ya kiwango kunamtokea mchezaji yoyote kwa mechi yoyote, mimi nimeajiriwa na Yanga ninafuata mkataba wangu unavyonituma," alisema Msuva.


Akizungumzia mchezo wao dhidi Azam wikiendi hii Msuva alisema mechi hiyo itakuwa ngumu kutokana na wapinzani wao kutokuwa na matokeo mazuri ya hivi karibuni.


"Tunaiheshimu Azam ni timu nzuri ina wachezaji wazuri ila sisi tumejipanga kuhakikisha tunapata ushindi, matokeo mabovu wanayoyapata yanaweza kuchangia mchezo huo kuwa mgumu zaidi."

Post a Comment

 
Top