BOIPLUS SPORTS BLOG

MANCHESTER, Uingereza
MANCHESTER United imebanwa mbavu na Burnley kwa kulazimishwa sare ya bila kufungana kwenye mchezo wa ligi uliofanyika Uwanja wa Old Trafford.

United walitawala sana mchezo huo kwa kulishambulia lango la Burnley lakini hawakuweza kupata bao ambapo mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic alikosa nafasi nyingi za kufunga.

Mwamuzi Mark Clutternberg alimtoa kwenye benchi Kocha Jose Mourinho baada ya kuongea maneno yakukosoa maamuzi ya refarii huyo huku pia akimlima kadi nyekundu kiungo Ander Herrera kutokana na kudhamiria kumkanyaga mchezaji mmoja wa Burnley.

Kikosi cha United kilichoanza leo ndicho kilichoisambaratisha Man City katikati ya Juma lililopita kwa ushindi wa bao 1-0 kwenye mchezo wa kombe la Capital One na kufanikiwa kuingia hatua ya robo fainali.

Matokeo mengine ya michezo ya ligi hiyo iliyochezwa leo ni kama ifuatavyo;

Sunderland 1-4 Arsenal
Middlesbrough 2-0  Bournemouth
Tottenham Hotspur 1-1 Leicester City
Watford 1-1 Hull City
West Bromwich 0-4 Man City

Post a Comment

 
Top