BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
UONGOZI wa klabu ya Yanga umewatangazia wanachama wake mkutano mkuu wa dharura uliopangwa kufanyika Jumapili Octoba 23 sehemu ambayo itatajwa siku chache zijazo kwa ajili ya kujadili maslahi mapana  ya Wanajangwani hao.

Mkutano huo unakuja siku chache baada ya Baraza la Michezo Tanzania BMT kuitaka klabu hiyo kufuata katiba yake kuelekea katika mabadiliko ya kiundeshwaji ambapo Mwenyekiti wake Yusuph Manji anataka kuikodi klabu hiyo kwa miaka 10.

Juzi Katibu mkuu wa BMT Mohamed Kiganja alinukuliwa akisema kuwa Yanga inapaswa kufanya marekebisho ya katiba yao ili iweze kufanya mabadiliko ya uendeshwaji wa klabu ambayo wanataka kuyaendea.

Taarifa inasema kuwa agenda za mkutano huo na mahali ambapo utafanyika zitawekwa wazi muda wowote kuanzia sasa huku wanachama wa klabu hiyo wakitakiwa kuhudhuria kwa wingi ili kupatikane maridhiano ya pamoja.

Wiki iliyopita uongozi huo ulitoa mkataba baina ya bodi ya wadhamini wa klabu hiyo na kampuni ya Yanga Yetu Limited kwa ajili ya kuikodisha nembo ya timu hiyo kwa miaka 10 kabla ya BMT kusema hawautambui mkataba huo kutokana na kutokidhi haja za kisheria.

Post a Comment

 
Top