BOIPLUS SPORTS BLOG

Akram Msangi, Shinyanga

NAHODHA wa Simba, Jonas Mkude ameweka wazi siri za wao kufanya vizuri kuwa ni kujituma na ushirikiano ndiko kunawabeba kwenye ligi kuu na kuendelea kuongoza ligi hiyo iliyoingia mzunguko wa 13 wakiwa na pointi 32.

Mkude ambaye timu yake haijapoteza mechi hata moja ikiwa imecheza mechi 12 aliiambia BOIPLUS kuwa wachezaji waliosajiliwa msimu huu wameongeza upinzani mkubwa ambao unaifanya timu hiyo iwe bora zaidi.

Mkude alisema kuwa upinzani huo unawapa changamoto kubwa kwa kila mchezaji kupambana ili kupata namba kwenye kikosi cha kwanza cha Simba chini ya Kocha Joseph Omog raia wa Cameroon.


Msimu huu Simba imewasajili Shiza Kichuya, Laudit Mavugo, Mzamiru Yassin, Fredrick Blagnon, Mohamed Ibrahim, Method Mwanjali, Jamal Mnyate, Janvier Bokungu na Musa Ndusha.

"Kiukweli tunapata ushirikiano mkubwa kutoka kwa viongozi, wanachana na mashabiki. Tunajitahidi kucheza kwa kiwango bora ili kupata matokeo mazuri yatakayowapa furaha kwani wote tumeunganishwa na Simba, tutajisikia faraja zaidi tukitwaa ubingwa msimu huu maana ni muda mrefu hatujatwaa kombe," alisema Mkude.

Post a Comment

 
Top