BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi Wetu, Dar
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli amemwomba msaada Mfalme Mohammed VI wa Morocco kufadhili ujenzi wa Uwanja wa michezo mjini Dodoma utakaogharimu kiasi cha dola 80 milioni.

Ombi hilo ameliwasilisha leo wakati wa halfa ya kumkaribisha Mfalme huyo aliyekuja nchini kwa ziara ya kibiashara na tayari amekubali ombi la Rais Magufuli.

Ujenzi huo utaifanya Tanzania kuwa na viwanja viwili vya kisasa, Uwanja wa Taifa uliopo jijini Dar es Salaam unaoingiza watu 60,000 uliojengwa wakati wa uongozi wa Rais Mstaafu, Benjamini Mkapa na huo utakaojengwa Dodoma ambako serikali kuu inahamia.

Serika ya Magufuli inapaswa kuhamia mjini Dodoma kuanzia Novemba Mosi ambapo sasa miundombinu ya kisasa itapaswa ijengwe huko na si Dar es Salaam ambayo itabaki na ofisi za kawaida.

Post a Comment

 
Top