BOIPLUS SPORTS BLOG

Sheila Ally
 Hemed Murutabose katikati akishangilia bao la kwanza lililofungwa na Raphael Alpha kushoto, kulia ni beki Haruna Shamte

STRAIKA Mrundi wa Mbeya City, Hemed Murutabose amecheza mechi tano mpaka sasa lakini hajafunga bao hata moja ingawa yeye anaamini kuwa muda wake wa kufunga bado haujafika na anachokifanya sasa ni kutoa pasi tu kwa wenzake ili wafunge.

Hemed ambaye leo Jumamosi amesababisha penati iliyozaa bao la kwanza lililofungwa na Raphael Alfa aliyepachika bao la pili pia kabla Ditram Nchimbi hajafunga bao la tatu katika ushindi wa bao 3-2 dhidi ya Majimaji, alisema anashindwa kufunga kirahisi kwani wachezaji wengi wa Tanzania hutumia nguvu kucheza na si akili.

"Aah mimi nacheza kwa kutafuta nafasi ya kufunga ila mimi si mchoyo nafika langoni nawapasia wenzangu walio kwenye nafasi nzuri zaidi za kufunga na wanafunga kirahisi tu, naamini nikipata nafasi nitafunga sana.

"Natakiwa kufunga lakini nakutana na wachezaji wengi wa Tanzania wanaotumia nguvu sana akili kidogo tofauti na ligi ya kwetu Burundi ligi sio ngumu ila ni nzuri sababu tunatumia akili sana nguvu kidogo sio kama huku," alisema Hemed.


Hemed alisema kuwa anaamini uwezo wake hapo baadaye utakuwa mkubwa kama ilivyo kwa Warundi wengine wanaokipiga hapa nchini kama Amissi Tambwe wa Yanga, Didier Kavumbagu aliyekuwa Azam pamoja na Laudit Mavugo wa Simba.

"Najuwa mwanzo ni mgumu, ila tuombe Mungu kila mtu ataonyesha kile alichonacho kwenye soka nitafanya vizuri kuliko hata hao. Tunaelekea mechi ya Yanga hivyo mashabiki watulie Yanga tumewaona na tunajuwa tupite wapi mpira wao sio mkubwa," alisema Hemed.

Post a Comment

 
Top