BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
WASANII wa vichekesho Mtanga, Bambo na Kiwewe watakuwepo kwenye tamasha la kuchangia damu lilioandaliwa na Taasisi ya Tegemeo Arts Group Tanzania litakalofanyika Desemba 25 kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.

Wachekeshaji hao wanaotamba na kipindi cha Ze Comedy kinachorushwa na kituo cha luninga cha East Africa Television ( EATV) wamekuwa kivutio kwa watazamaji wengi kutokana na lafudhi za makabila yao ambayo hutumia wakiwasilisha Ujumbe kwa jamii.


Tamasha hilo lina dhamira ya kuchangia damu kwa hiari kwa ajili ya kusaidia wagonjwa kwenye hospitali mbalimbali mkoani Morogoro kutokana na uhaba uliopo licha ya kuwepo hitaji kubwa baada ya ajali nyingi kuripotiwa kutokea mara kwa mara mkoani humo.

Mbali na wachekeshaji hao tayari Afande Sele,Bendi ya FM Academia  Hadija Kopa, Mwanahawa Ally, Hadija Yusuph na Wasanii wa kadhaa wa Singeli wameshathibitisha kushiriki tamasha hilo.


Msanii Abbas Kinzasa '20%' alitarajiwa kuthibitisha uwepo hii leo lakini kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wake alishindwa lakini jitihada bado zinafanyika ili nae awepo miongoni mwa washiriki.

Post a Comment

 
Top