BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi Wetu
SIMBA leo Jumamosi imeshinda bao 3-0 dhidi ya Mwadui FC katika mechi iliyopigwa Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga lakini Wachimba Almasi hao wamesema kuwa wamefungwa kwa uzembe wao.

Matokeo hayo yamewafanya Simba kuwaacha mbali watani zao Yanga kwa kufikisha pointi 32 huku Yanga wanaoingia dimbani kesho Jumapili kucheza na Mbao wamekusanya pointi 24. Mwadui wao wanashika nafasi ya 12 wakiwa na pointi 13.

Beki wa Mwadui FC, Joram Mgeveke alisema kuwa wapinzani wao walifanikiwa kutumia vizuri nafasi walizozipata tofauti na wao ambao walipoteza umakini huku viungo wa Simba wakichezea dimba watakavyo.


"Tumefungwa kutokana na sisi wenyewe tu kukosa umakini ukiangalia kipindi cha kwanza ilibidi tuwafunge kabla ya wao kutufunga ila hatukufanikiwa, timu nzima hatukuwa makini si uliona watu katikati walicheza watakavyo wao.

"Makosa madogo madogo tuliyoyafanya ndio wenzetu wametumia nafasi hizo ndio maana kipindi cha pili Simba walikuwa wanacheza kwao kwani waliona wasingeweza kuongeza goli, maana na sisi tulianza kupambana ingawa hakukuwa na mafanikio yoyote," alisema Mgeveke.

Post a Comment

 
Top