BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi wetu
MWANACHAMA wa timu ya Simba Mzee Hajji Mkelo amefariki duniani leo asubuhi baada ya mshtuko wa mabomu ya machozi yaliyopigwa uwanjani kutokana na vurugu zilizojitokeza kwenye mchezo wa Simba na Yanga uliopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mwanachama huyo wa tawi la Simba Dumila Morogoro ambaye alisafiri na wenzake kuja kutazama mchezo huo ambao ulisimama kwa dakika kadhaa baada ya mabomu kupigwa uwanjani hapo kufuatia vurugu zilizotokea ambapo mashabiki waling'oa viti baada ya kutoridhishwa na maamuzi ya refarii.

Mzee Mkelo alikimbizwa hospitali baada ya hali kuwa mbaya saa 10 alfajiri kabla ya kufariki dunia saa 2 asubuhi ya leo.

Post a Comment

 
Top