BOIPLUS SPORTS BLOG

Zainabu Rajabu,Dar
Shiza Kichuya akiwa mbele ya picha ya Mafisango baada ya kuifungia Simba bao, nyumba yake ni Janvier Bokungu


KINARA wa mabao kwenye Ligi Kuu ya Vodacom, Shiza Kichuya anayeichezea Simba ameweka wazi kuwa uwezo wake wa kufunga mabao ndani ya timu hiyo ni kutokana na taswira ya marehemu Patrick Mafisango anayoiona kila mara mawazoni mwake.

Mafisango alifariki dunia Mei 17, 2012 kwa ajali ya gari akiwa ni miongoni mwa wachezaji waliotegemewa ndani ya Simba na inaelezwa kwamba hadi sasa pengo lake bado halijazibwa kutokana na uwezo mkubwa aliokuwa nao mchezaji huyo.

Mara kadhaa Kichuya amekuwa akiikimbilia picha ya Mafisango anapofunga bao na ameelezea kuwa kitendo hicho ni moja mambo ya kuenzi kazi za Mafisango alipokuwa ndani ya Simba enzi za uhai wake.


Marehemu Patrick Mafisango

"Ni mtu ambaye nilitamani siku moja nifanye naye kazi, ndiye anayenifanya niwe na juhudi ya kujituma na kutokata tamaa katika maisha yangu ya soka," alisema Kichuya.

Kichuya ambaye amefikisha mabao saba mpaka sasa amewaahidi Wanasimba kufanya mambo makubwa zaidi ili kurudisha heshima ya klabu hiyo iliyokuwa imepotea kwa muda mrefu kama alivyokuwa akifanya Mafisango.

Post a Comment

 
Top