BOIPLUS SPORTS BLOG

Kampala,Uganda
KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya Uganda 'The Cranes' Sredojovic Milutin 'Micho' amekitaja kikosi cha nyota 19 kitakachoweka kambi nchini Togo huku akimjumuisha straika wa zamani wa Simba Hamis Kiiza na kumuacha Emmanuel Okwi ambaye aliwahi kung'aa na wekundu hao pia.

Kikosi hicho  kinasafiri usiku wa leo kuelekea Lome nchini humo ambapo watacheza mechi moja na wenyeji wao  'Sparrow Hawks' keshokutwa Jumanne kabla ya kuwafuata Ghana 'Black Stars' katika mechi ya kwanza ya kufuzu michuano ya kombe la dunia itakayofanyika nchini Russia mwaka 2018, mtanange utakaopigwa  Octoba 8.

Okwi ametemwa kutokana na kutopata sana nafasi  kwenye klabu yake hali iliyomfanya Micho kumchinjia baharini na kumpa nafasi Kiiza ambaye yupo katika ubora wa juu nchini Afrika Kusini.

KIKOSI KAMILI:

MAKIPA
Denis Onyango, Jamal Salim na Ochan Benjamin.

MABEKI
Wadada Nicholas, Iguma Denis, Isinde Isaac, Juuko Murshid, Ochaya Joseph na Godfrey Walusimbi.

VIUNGO
Waswa Hassani, Kizito Geofrey, Aucho Khalid, Mawejje Tony pamoja na Moses Oloya.

WASHAMBULIAJI
Kizito Luwagga, Miya Farouk, Massa Geoffrey, Kiiza Hamis na Sentamu Yunus.

Post a Comment

 
Top