BOIPLUS SPORTS BLOG

Akram Msangi, Shinyanga
Kiungo Mzamiru Yassin kushoto akimiliki mpira mazoezini mbele ya mlinzi Janvier Bokungu na Meneja Mussa Mgosi

Ame Ally 'Zungu' alipata  maumivu ya nyama za paja, hata hivyo daktari wa timu hiyo Yassin Gembe aliiambia BOIPLUS kuwa wanaendelea kumhudumia na jibu la kwamba atacheza au hatocheza litatolewa kesho

Mohamed Hussein 'Zimbwe Jr' akionyesha ufundi wa kuuchezea mpiraAhmad Juma kushoto akiuzuia mpira usimfikie Abdi Banda kulia, wachezaji hao wote wawili bado hawajajihakikishia nafasi katika kikosi cha kwanza. Vita ya namba katika kikosi hicho ni kubwa sana

Kiungo Mwinyi Kazimoto akimchungulia kipa Vicent AngbanAngban akionyesha uwezo unaomfanya aendelee kuaminika katika kikosi cha kwanza

Kipa namba mbili, Manyika Peter Jr anapambana kuhakikisha anampoka namba Angban baada ya kuonyesha uwezo mkubwa mazoeziniKocha Joseph Omog akizungumza jambo na nahodha Jonas Mkude. Pambano la Simba na Stand United limekuwa gumza katika mitaa ya mji wa Shinyanga huku mashabiki wengi wa Stand wakionyesha kujiamini watamtuliza Mnyama ambaye hajafungwa tangu kuanza kwa ligi kuu.

Post a Comment

 
Top