BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
Beki wa kushoto wa Yanga Oscar Joshua (kulia) akiwa mazoezini kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbao FC utakaopigwa jumapili hii katika dimba la Uhuru

 Kiungo Thaban Kamusoko akimuonyesha ufundi Donald NgomaBeki wa kati Andrew Vicent 'Dante' amekuwa tegemeo katika safu ya ulinzi ya kikosi cha wanajangwani hao

Mazoezi ya leo yaliongozwa na kocha msaidizi Juma Mwambusi.

Wakali wa mabao Donald Ngoma (kushoto) na Obrey Chirwa, je, Mbao wataweza kuzuia kasi yao ya kupachika mabao?

Kocha wa makipa wa Yanga Juma Pondamali akimpa maelekezo kipa namba tatu wa timu hiyo Beno Kakolanya ambaye alinukuliwa na BOIPLUS jana kuwa bado anapambana na anaamini atapata nafasi katika kikosi cha kwanza.

Kinda Yusuph Mhilu akipatiwa matibabu baada ya kuumia akiwa mazoeziniMawinga teleza......Simon Msuva na Juma Mahadhi, hawa wamekuwa chanzo cha mashambulizi mengi ya wanajangwani hao huku Msuva akiwa ameshapachika mabao matano hadi sasa

Deus Kaseke, Mahadhi na Msuva wakijadiliana jambo Winga Geofrey Mwashiuya 

Kelvin Yondan (mwenye fulana nyeusi) alishindwa kufanya mazoezi kutokana na kuwa na maumivu ya vidole.

Post a Comment

 
Top