BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
BAADA ya kufanikiwa kufunga bao lake la kwanza kwa timu yake Yanga Kocha Hans Pluijm amemwagia sifa mshambuliaji wake Obrey Chirwa kutokana na uvumilivu wake licha ya kupata changamoto kutoka kwa mashabiki ambao wamekuwa wakimsema vibaya.

Chirwa ndiye mchezaji ghali zaidi kwenye ligi kuu ya Vodacom baada ya kusajiliwa na mabingwa hao toka FC Platinum kwa ada ya milioni 200 lakini kuchelewa kufunga goli kulifanya mashabiki wa timu hiyo kukosa imani nae huku katibu wa Baraza la wazee wa klabu hiyo Mzee Ibrahim Akilimali akikiri kuwa Yanga waliingia mkenge kumsajili mchezaji huyo.

Mholanzi huyo alisema kuwa ana matarajio makubwa kutoka kwa Chirwa kutokana na umahiri wake pamoja na uvumilivu aliokuwa nao licha ya kupigiwa kelele na mashabiki wa Yanga na ameonesha uweledi mkubwa kama mchezaji wa kimataifa.

"Alikuwa kwenye presha kubwa ni mchezaji mgeni ambaye amekuja kwenye timu yenye mashabiki wengi kwahiyo alikuwa anapita katika kipindi kigumu ila kwa kufunga bao lile litampunguzia presha na kurudi kwenye kiwango chake," alisema Pluijm.

Kocha huyo alisema kipa Ally Mustapha 'Barthez' hakuwekwa benchi kutokana na matokeo ya mechi dhidi ya Simba ila kwakua timu hiyo imesajili makipa watatu na katika mechi wanapangwa wawili mmoja anaanza na mwingine anakua benchi kwahiyo hakuna tatizo na mlinda mlango huyo.

"Hakuna tatizo na Barthez na katika mechi lazima makipa wawili wawepo kwahiyo yeye alipumzishwa kama inavyokuwa kwa Beno(Kakolanya) hivyo hakuna tatizo lolote," alisema Pluijm.

Mholanzi huyo alisema kuwa bado wapo kwenye mbio za kutetea ubingwa wao licha ya wapinzani wao Simba kuwa vinara ila kwakua bado wana michezo 23 ambayo wakicheza vizuri wanaweza kuibuka tena mabingwa msimu huu.

Post a Comment

 
Top