BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
LICHA ya Azam kuwa na matokeo mabovu kwenye michezo yake ya ligi katika siku za karibuni timu Yanga haitawadharau katika mechi yao ya Jumapili kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Katika michezo nane iliyoshuka dimbani Azam imeshinda mitatu imepoteza mitatu na kwenda sare katika mechi mbili hali inayooneka kuwa wanaweza kupoteza dhidi ya mabingwa hao lakini Yanga wenyewe wanasema wanawaheshimu na wanaamini mchezo huo utakuwa mgumu.

Kocha wa mabingwa hao watetezi Mholanzi Hans Pluijm alisema Azam bado siyo timu ya kubeza kwa matokeo ya michezo nane anaamini wanao wachezaji wazuri wanaoweza kubadili matokeo muda wowote kwahiyo wataingia uwanjani kwa tahadhari kubwa.

"Azam siyo timu ya kubeza licha ya kutokuwa na matokeo mazuri hiyo haitupi uhakika wa kushinda mchezo kirahisi tutaingia uwanjani kucheza kama kawaida bila kudharau," alisema Pluijm.

Mholanzi huyo alisema pia kukutana na timu ambayo ipo kwenye wakati mgumu wakati mwingine sio vizuri kwakua wanakamia na kutaka kupata matokeo kwa hali yoyote kitu ambacho wanapaswa kuwa makini nacho katika mchezo dhidi ya 'Wana lamba lamba' hao.

Yanga inashika nafasi ya nne baada ya kujikusanyia alama 14 kutokana na michezo saba iliyotelemka dimbani huku Azam wakiwa nafasi ya nane baada ya kujikusanyia pointi 11 kibindoni katika mechi nane.

Post a Comment

 
Top