BOIPLUS SPORTS BLOG

Zainabu Rajabu,Dar

KOCHA Mkuu wa Yanga, Hans Pluijm amesema kwamba wanashindwa kupata matokeo mazuri kwenye mechi za ugenini kwasababu timu hizo zinacheza kwa kukamia ili kupata sifa za kuifunga Yanga.

Yanga imeshindwa kupata matokeo ya kuridhisha kwenye mechi zao za awali hasa za mikoani ambapo imecheza mechi mbili za Kanda ya Ziwa, ilishinda mechi dhidi ya Mwadui na ikapoteza mechi yao na Stand United zote za Shinyanga.

Akizungumza na BOIPLUS, Pluijm alisema wanapocheza ugenini wanakutana na changamoto kwa baadhi ya timu kutaka kuvuna pointi katika viwanja vyao vya nyumbani.

"Inakuwa ngumu sana kupata pointi tatu kwenye viwanja vya mikoani kwa mechi tunazocheza kutokana na kila timu kutaka kuifunga Yanga ili kupata umaarafu, timu ambazo tunakutana nazo ni ngumu na zimejipanga kucheza kwa malengo na kutubana kushindwa kucheza mpira wa pasi," alisema Pluijm.

Yanga ambayo imefikisha pointi 15 imetua leo asbuhi jijini Mwanza kwa ajili ya mechi yao ya kesho dhidi ya Toto African, mechi itachezwa uwanja wa CCM Kirumba na baada ya hapo itaelekea Kagera kucheza na Kagera Sugar.

Yanga haijasafiri na nyota wake Juma Abdul, Ally Mustapha 'Barthez' na Malimi Busungu ambaye ni kama amepoteza namba kwenye kikosi hicho.

Post a Comment

 
Top