BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
SHIRIKISHO la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limetoa ufafanuzi kuhusu kutumika kwa Uwanja wa Kambarage badala ya Mwadui Complex kwenye mchezo kati ya Mwadui FC dhidi ya Simba utakaofanyika kesho kutokana na dimba hilo kushindwa kuhimili wingi wa Mashabiki wa Wekundu hao.

Uwanja wa Kambarage umekuwa ukitumika kwa Mwadui inapokutana na timu za Simba na Yanga kutokana na kuwa na idadi kubwa ya Mashabiki kutoka mkoani humo na mikoa ya jirani.

Ofisa Habari wa TFF Alfred Lucas alisema kuwa Uwanja huo majukwaa yake ni madogo kulinganisha na idadi kubwa ya mashabiki kutoka mikoa ya Mwanza, Singida wengine kutoka jijini Dar es Salaam hali inayoonyesha dimba hilo haliwezi kutosha.

"Uwanja wa Kambarage ndiyo utakaotumika kwa mechi ya Mwadui dhidi ya Simba kwavile ni mkubwa ambao utaweza kuchukua mashabiki wengi," alisema Lucas.

Simba wataingia kwenye mchezo huo wakiwa ndio vinara wa ligi wakiwa na pointi 29 baada ya kushuka dimbani mara 11.

Post a Comment

 
Top