BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
DANADANA za Safari ya winga wa Azam Farid Mussa kuelekea nchini Hispania kucheza soka la kulipwa zinaelekea kufika kikomo baada ya Wanalamba lamba' hao kukamilisha suala hilo kwa zaidi ya asilimia 90.

Azam tayari wameshawatumia hati ya uamisho ya kimataifa (ITC) kwa klabu ya Tenerrife inayoshiriki ligi daraja la kwanza ambayo imekuwa ikihitaji huduma za winga huyo ambaye amekuwa katika kiwango bora kwa sasa.

Ofisa Habari wa Azam Jaffar Iddi Maganga alisema tayari timu hiyo ya Hispania inamtafutia winga huyo kibali cha kufanya kazi nchini humo ili kumwezesha kukipiga katika timu hiyo kwa mkopo wa muda mrefu.

"Suala la Faridi lipo kwenye hatua nzuri muda si mrefu winga huyo ataelekea nchini Hispania kwakua kila kitu kinaenda sawa, tunasubiri kibali cha kazi kikipatikana hata kesho anasafiri," alisema Jaffar.

Jaffar alisema pia baada ya kambi ya timu ya Taifa kuvunjwa kufutia kuahirishwa kwa mchezo dhidi ya Ethiopia wachezaji wote wamerudi kambini kujiandaa na mchezo wa Stand United utakaopigwa wiki ijayo kwenye uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga.

Aidha Msemaji huyo alisema mechi zote ambazo Azam watacheza katika uwanja wake wa nyumbani wa Azam Complex zitachezwa saa moja usiku kutokana na utaratibu waliojiwekea.

Post a Comment

 
Top