BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
KIUNGO Mkongwe wa timu ya Ndanda FC ya mkoani Mtwara Shija Mkina amewabwatukia wachezaji wenzake kufutia kupigo cha bao 1-0 walichokipata toka kwa African Lyon jana kwenye mchezo wa ligi kuu uliofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mkina alioneka kukasirishwa na matokeo ya mchezo huo ambao anasema wachezaji wenzake waliwadharau Lyon na hawakuwa makini uwanjani ndiyo maana wakapoteza nafasi nyingi hali iliyosababisha kuambulia kipigo kutoka kwa wenyeji wao.

Mkina ameiambia BOIPLUS kuwa walicheza kwa dharau huku vichwani mwao wakiamini wanaweza kuibuka na ushindi tena wa mabao mengi kitu kilichopunguza umakini miongoni mwao na kupelekea kipigo ambacho hawakustahili kukipata.

"Tulicheza hovyo sana mechi hii, tuliamini tunaweza kuwafunga Lyon kirahisi sana tukasahau kuwa mpira una matokeo matatu.

"Kitu kilichonikera hadi kukasirika vile ni kupoteza mechi dhidi ya timu dhaifu, ilitakiwa tushinde mchezo ule kwavile bado tuna mechi ngumu ugenini," alisema Mkina.

Mchezaji huyo wazamani wa Simba aliyeonekana kuwa na jazba baada ya kumalizika mchezo huo alisema walifanya kikao kifupi kwenye vyumba vya kubadilishia nguo ili kukumbushana majukumu yao wawapo uwanjani kwa sababu mechi bado ni nyingi ambazo wakijipanga wanaweza kufanya vizuri.

"Unajua vijana wakati mwingine wanajisahau na kujiamini kupita maelezo mpaka wanashindwa kutimiza majukumu yao, tulikuwa kwenye kikao kuweka mambo sawa," alimalizia Mkina.

Post a Comment

 
Top