BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
GOLIKIPA nambari moja wa Mtibwa Sugar Saidi Mohamed 'Nduda' aliyekuwa ameumia goti lililomuweka nje ya uwanja kwa mwezi mmoja sasa amepona na anatarajia kurejea uwanjani wiki mbili zijazo.

Nduda alishuhudia timu yake ikilala kwa mabao 3-1 toka kwa mabingwa watetezi Yanga mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam ambapo 'Wakata miwa' hao walishindwa kufurukuta mbele ya vijana hao Wa Jangwani.

Kipa huyo ameiambia BOIPLUS kuwa tayari ameanza kufanya mazoezi na wenzake kwa muda wa wiki sasa akiendelea kupata maelekezo ya madaktari wa timu hiyo kabla ya kurejea kwenye milingoti mitatu baada ya wiki mbili.

"Namshukuru Mungu naendelea vizuri, nilikuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya mwezi sasa lakini nimeshaanza mazoezi na wenzangu na kwa mujibu wa taarifa za madaktari naweza kurudi uwanjani ndani ya wiki mbili," alisema Nduda.

Katika mchezo wa jana dhidi ya Yanga Mtibwa walimchezesha kipa Benedict Tinocco ambaye msimu uliopita alikuwa kwa mabingwa hao akiwa kipa namba tatu ambapo hakufanikiwa kudaka hata mechi moja.

Post a Comment

 
Top