BOIPLUS SPORTS BLOG

Sheila Ally, Dar
KIUNGO mkongwe wa Ruvu Shooting, Shaban Kisiga 'Marlone' ameweka wazi siri ya ubora wake pamoja na baadhi ya wakongwe wenzie kuwa ni kujitunza, kujituma kwenye mazoezi pamoja na kuachana na starehe.

Marlone ambaye amewahi kuichezea Simba, ameonekana kuwa katika ubora wake na kumudu kucheza mechi kwa dakika 90 bila kuchoka tofauti na baadhi ya wachezaji ambao ni chipukizi.

Akizungumza na BOIPLUS, Marlone alisema kuwa wachezaji wengi wamekuwa wakijisahau kwa kufanya mambo mawili kwa wakati mmoja pasipo kupangilia muda wa kufanya mazoezi na starehe.


"Unajuwa kila kitu kina wakati wake, wachezaji wengi hujisahau ila wanapaswa kutenga muda na kujitambua pamoja na kufanya mazoezi ili miili yao iwe na utayari," alisema Marlon.

Akizungumzia changamoto ya Ligi Kuu ya Vodacom alisema kuwa; "Nadhani kila mtu afanye kazi yake, TFF, Makocha, viongozi wa timu, wachezaji na waamuzi asiwepo wa kumuingilia mwenzake, nadhani kwa kufanya hivi ligi itachezwa kwa haki.

"Ligi ni ngumu mno na ndiyo maana ukiangalia hata pointi za timu hazijapishana sana, haki ikiwepo basi kila timu itapata matokea stahili kuliko timu inajiandaa ila inavunjwa nguvu uwanjani kwa kuonewa," alisema Marlon.


Post a Comment

 
Top