BOIPLUS SPORTS BLOG

MANCHESTER, Uingereza
TIMU za Manchester United na Chelsea zimeingia kwenye vita ya kumwania mshambuliaji kinda 
Moussa Dembele mwenye umri wa miaka 20 raia wa Ufaransa anayekipiga  Celtic kwa dau la pauni  40 Milioni.

Taarifa zinasema Man United na Chelsea zinaungana na Real Madrid katika kumwania Straika huyo fundi wa kucheka na nyavu aliyehamia Celtic akitokea Fulham.

Dembele amefunga mabao 15 katika michuano yote msimu huu yakiwemo mabao mawili aliyowafunga Manchester City kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya na magoli 7 katika ligi ya Scotland.

Straika huyo ameonesha umahiri wa kufumania nyavu kutokana na kasi, nguvu na uwezo wa kuwapita mabeki. 

Madrid huenda ikawa na nafasi ndogo katika kumsajili kinda huyo baada ya kukumbwa na adhabu ya kufungiwa kusajili hadi mwaka 2018 hivyo kupelekea United na Chelsea kuwa katika nafasi nzuri zaidi kumpata nyota huyo.

Post a Comment

 
Top