BOIPLUS SPORTS BLOG

NAIROBI,Kenya
KOCHA wa zamani wa timu ya Azam FC Muingereza Stewart Hall amesaini mkataba wa miaka miwili kuifundisha FC Leopards ya Kenya ambayo mwenendo wake hauridhishi sana katika ligi hiyo.

Katika vipindi viwili tofauti Muingereza huyo aliifundisha Azam na akiikuta timu kwenye wakati mgumu lakin mara zote  akifanikiwa kuwarudisha kwenye mstari kabla ya kutimuliwa mambo yalipoenda kombo.

Hall na benchi lake zima la ufundi lilifungashiwa virago mwezi Juni mwaka huu kutokana na mwenendo wa kusuasua hali iliyosababisha mabosi wa Wanalambalamba hao uvumilivu kuwashinda na kuwatimua kabla ya fainali ya kombe la FA dhidi Yanga waliyolala mabao 3-1 kwenye uwanja wa Taifa.

Hall ameikuta Leopards ikiwa nafasi ya 12 kwenye msimamo wa ligi ya Kenya baada ya kujikusanyia alama 30 katika michezo 26 iliyoshuka dimbani.

Tusker ndiyo vinara wa ligi hiyo wakiwa na alama 51 wakifuatiwa na Gor Mahia wenye alama 44 baada ya michezo 26 huku Sofapaka wakiburuza mkia wakiwa na pointi 16.

Post a Comment

 
Top