BOIPLUS SPORTS BLOG

Karim Boimanda, Dar
Amissi Tambwe jana alihitimisha ushindi wa mabao 3-0 walioupata Yanga dhidi ya Mbao FC kwa kutupia bao la tatu katika kipindi cha pili.

Mpira huo ulianzia kwa Haruna Niyonzima (kushoto) ambaye aliupenyeza mpira katikati ya walinzi wa Mbao na mpira kumkuta Tambwe

Tambwe aliupokea mpira huo kiufundi kabla hajamchambua kipa Emmanuel Mseja anayeonekana kuishia kuukodolea macho mpira ukielekea nyavuni

Hapa kazi imeshakamilika, Tambwe anashangilia kuelekea kwa mashabiki wa Wanajangwani hao

Maelfu ya mashabiki wa Yanga wakilipuka kwa shangwe baada ya bao hilo la tatu

Post a Comment

 
Top